Vodacom Yazindua Dawati La Huduma Kwa Wateja Wasioona. Dar es Salaam – Januari 24, 2024. Katika jitihada za kuhakikisha inatengeneza usawa na ujumuishi wa mazingira bora ya ufikiwaji wa huduma zake na wateja wake wote nchini, kampuni ya teknolojia na mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC imezindua dawati la huduma kwa wateja kwa watu wenye ulemavu jijini Dar es Salaam. Akizungumza wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye duka la huduma kwa wateja lililopo makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Bw. Philip Besiimire amesema kuwa siku zote kampuni inajitahidi kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma zake kuhakikisha zinawafikia na kuwanufaisha wateja wote bila ya ubaguzi.
January
25
2024
0Comment